Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Longido ndugu Stephen A. Ulaya leo tarehe 13 Januari 2023 ameongoza zoezi la ugawaji wa vishkwambi kwa maafisa elimu kata,wakuu wa shule za msingi na Sekondari katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido
Aidha akikabidhi vishkwambi hivyo kwa watumishi hao Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Longido ndugu Khamana Simba amewaasa watumishi kuvitunza vishikwambi hivyo pamoja na kuvitumia kwa namna bora kwani kwa kufanya hivyo vitawasaidia sana katika dhana nzima ya kujifunza na kujifunzia na kuongeza tija na ufaulu wa wanafunzi kwani kwa kutumia vishkwambi hivi tofauti na kurahisisha mawasiliano kidijatali pia vitawasaidia kupata miongozo mbali mbali ya elimu.
Aidha ndugu Khamana Simba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake mama Samia Suluhu Hassan kwa kuona ipo haja ya kurudisha vishkwambi hivyo mashuleni ikiwa na lengo la kuboresha elimu kwa njia ya mtandao.
Pamoja na zoezi hilo ndugu Khamana Simba ameongoza zoezi la usainishwaji wa mkataba kwa walimu wa shule za msingi, sekondari pamoja na Maafisa Elimu kata, mkataba huo ukiwa na malengo mahususi matatu ikiwemo kuhakikisha wanafunzi hususani wa shule za msingi wanajua vema kusoma, kuhesabu, na kuandika wafikapo darasa la tatu ili upunguza wimbi la watoto wasio jua kusoma kuandika na kuhesabu pia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuweka mkazo katika kujifunza kingereza Kuanzia darasa la tatu na kuendelea, pia kila mwalimu kujiwekea mikakati iliyo thabiti na malengo binafsi ya kupandisha ufaulu yaani daraja A, B, C na kuondokana kabisa na daraja F
Nae Afisa Elimu Msingi mwalimu Deusdedit Bimbalilwa Kwa niaba ya walimu ameishukuru Serikali kwa kuona sababu ya kuchagua idara ya Elimu kwenye ugawaji wa vishkwambi na ameahidi kuvitunza kama miongozo inavyosema.
'Ndugu walimu tutumie vishkwambi hivi kwa umakini na kuvitunza "alisema mwalimu Gilbert Sombe Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM