Mkurugenzi atimiza ilani ya ccm
Waheshimiwa wa Kata mbalimbali wa Kamati ya fedha walifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Halmashauri ili kujiridhisha.
Waheshimiwa Madiwani hao walitembelea na kukagua miradi inayopatikana maeneo ya Namanga,Kimokouwa,Longido,Tingatinga na Mradi mkubwa wa maji Olmology.
Miradi hiyo iliyokaguliwa ni Mradi mkubwa wa maji kutoka Mto Simba hadi Longido mjini,Kukamilika ujenzi wa Zahanati ya Kimokouwa ,Ujenzi wa miundombinu ya Mnada wa MIVARF,Mradi wa ujenzi wa jingo la x-ray Kituo cha Afya Longido,kutembelea mradi wa maji Tingatinga Ngereyani,na Ujenzi wa nyumba ya walimu Six in one ,ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa choo cha matundu 8 na choo cha matundu 2 katika shule ya Sekondari Tingatinga.
Aidha mradi uliokamilika ni Ujenzi wa Zahanati ya Kimokouwa ,ikiwa wa ujenzi wa Jengo la Zahanati,ujenzi wa choo,na uwekaji wa maji,na ujenzi wa Placenta Pit uliotumia jumla ya shilingi 59,131,854..Changamoto iliyopo ni Zahanati kukamilika lakini haina nyumba za Watumishi.
Baadhi ya miradi ambayo ipo katika hatua nzuri za ukamilishwaji ni Ujenzi wa programu ya MIVARF,ambapo ni ujenzi wa mazizi ya ng’ombe ,ujenzi wa vyoo pamoja na jingo la utawala.Mradi huo unagharimu jumla ya shilingi 314,078,944.80 na mpaka sasa Halmashauri imechangia jumla ya shilingi 20,000,000.Mradi mwingine ambao upo kwenye mwendelezo ni Ujenzi wa jingo la x-ray room katika kituo cha Afya Longido.
Majibu hayo yalitolewa Bungeni mjini Dodoma
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM